Header Ads

Maamuzi ya Madiwani Makete leo, Yupo mtumishi aliyefukuzwa kazi

Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe Hii leo limetoa maamuzi dhidi ya mashauri mbalimbali ya kinidhamu ya watumishi kadhaa ndani ya halmashauri hiyo
Mashauri hayo yamefikishwa kwenye baraza hilo kwa ajili ya maamuzi baada ya baraza kujigeuza kama kamati na kujadili na hatimaye kutoka na maamuzi Ikiwemo kufukuzwa kazi
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh Egnatio Mtawa ndiye aliyetoa taarifa ya maamuzi hayo mbele ya baraza
Akitilia mkazo maamuzi hayo mwenyekiti wa halmashauri Mh Mtawa amesema wamepitia kwa makini mashauri hayo ya kinidhamu kuhakikisha haki inatendeka kwa kila mtumishi huku akiwahakikishia kuwa watumishi wote wa halmashauri wapo kwenye mikono salama katika baraza la madiwani linalotenda haki kwa kila mmoja

No comments

Powered by Blogger.