'Expansion joint' Ya Mabweni ya Chuo ya UDSM Yazibwa
Wakala
wa Majengo nchini (TBA) umefanya ukarabati wa majengo ya mabweni ya
chuo kikuu cha Dar es salaam ambayo hivi karibuni yalionekana kuweka
nyufa.
Vyombo
vya habari vilivyofika kwenye eneo hilo vilikuta tayari mafundi
wameshaweka plasta ili kuziba nyufa hizo, ambazo Mkurugenzi Mkuu wa TBA
Elius Mwakalinga alisema zimesababishwa na 'expansion joint' ambayo ni
kitu cha kawaida kwenye ujenzi.
Hivi
karibuni kulisambaa picha za majengo zikionyesha kuwa na nyufa, huku
yakiwa hayajamaliza mwaka tangu yakabidhiwe na kuanza kutumika na
wanafunzi, kitendo kilichosababisha mpiga picha hizo ashikiliwe na
polisi.
Picha zinazoonyesha nyufa hizo zikiwa zimezibwa
No comments