Baada ya kuhojiwa uraia, Askofu Niwemugizi azungumza na Rais Magufuli
Baada
ya kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji kuhusu uhalali wa uraia wake Askofu wa
Jimbo la Ngara - Rulenge, Severine Niwemugizi ameeleza kwamba
amezungumza na Rais John Magufuli.
Jana,
askofu huyo alikaririwa akisema amehojiwa mara mbili na Uhamiaji katika
kile kinachoelezwa ni utata wa uraia wake huku akieleza kuwa amezaliwa
wilayani Biharamulo mkoani Kagera.
Alipoulizwa
kama mazungumzo hayo na Rais Magufuli ni baada ya taarifa za kuhojiwa
na Uhamiaji, Askofu Niwemugizi alijibu huku akianza kwa kucheka, “Hahahahaha!! Ni kweli Rais kataka kujua hasa kuna nini, yeye amesema atalifuatilia na kukiwa na... nitamfahamisha.”
Askofu
huyo ambaye Septemba mwaka huu aliibua mjadala wa Katiba Mpya na kusema
kuwa yuko tayari kuitwa mchochezi endapo kundi la watetezi wa haki za
binadamu watachukuliwa kama wachochezi alisema kuhojiwa huko
hakutamrudisha nyuma katika misimamo yake, “Siwezi kurudi nyuma, nimetumwa na Kristo, Nabii anaweza kupendwa au kuchukiwa na mimi siwezi kunyamaza.”
Askofu Niwemugizi aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) alisema, “Mimi nazungumza lakini kuna Watanzania wengine wanazungumza sana. Lakini mimi kuhojiwa mara mbili hakutaninyamazisha.”
Ujumbe aliouweka Facebook, unasema, “Nasali
Ee Bwana, unihukumu, unitetee kwa taifa lisilo haki, uniokoe na mtu wa
hila asiye haki. Kwa kuwa wewe ndiwe Mungu uliye nguvu zangu; kwa nini
umenitupa?
No comments