TFDA YATOA TAHADHARI KUHUSU BIDHAA
Afisa afya Wilaya ya Makete Ndg.Boniface Sanga
Wafanyabiashara Wilayani Mkoani Njombe wametakiwa
Kutohifadhi Mafuta ya Kupikia,Chumvi,Maji, pamoja na Unga kwenye jua ili bidhaa hizo zisipoteza ubora wake.
Agizo hilo limetolewa na Mamlaka ya Chakula
na Dawa Nchini (TFDA) Kupitia kwa Afisa afya Wilaya ya Makete BONIFACE SANGA amesema
bidhaa hizo hazitakiwi kukaa kwenye jua ilihali zinatakiwa kukaa sehemu ambayo
ina ubariki ili zisipoteze thamani yake na kuleta madhara kwa binadamu.
‘‘Masharti ya hizo Bidhaa inatakiwa kukaa
kwenye Baridi siyo kukaa juani ili zisiondolewe uthamani wake na kuleta madhara
kwa watumiaji wa bidhaa hizo na mfanya
biashara yoyote ambaye atakiuka utaratibu huo atafungiwa biashara yake au
bidhaa zake zitateketezwa kwa moto’’ Amesema Bonifasi sanga.
Hata hivyo BONIFACE SANGA amesema ndani ya
siku kumi na nne [14] Idara ya Afya Wilaya ya Makete watapita Kufanya Ukaguzi kwa wafanyabiashara
ambao wanaweka bidhaa hizo kwenye jua endapo mfanyabiashara yeyote atakiuka
utaratibu huo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Hatua hizo ni kutokana na sheria ya mwaka
2003 kifungu namba 19 sura ya 219 inayosimamia uharibifu wa bidhaa hizo katika maeneo ya biashara na
kuweka kwenye jua ambapo virutubisho
vyake vinaondolewa kwa kukaa kwenye jua.
Mamlaka ya chakula na dawa Tanzania TFDA kwa Kushirikiana na Idara ya Afya Wilaya
ya Makete imewaomba wananchi wilaya kuwa makini kutumia bidhaa hizo na Wafanyabiashara
kuzingatia Taratibu na Sheria zinazotolewa na mamlaka husika ili kufanya Biashara
kwa Uhuru.
No comments