JAMAA AITA POLISI ASAIDIWE KUTULIZA BALAA LA NGURUWE MTATA.
Maafisa wa polisi hupokea simu zisizo za kawaida za watu
wakiomba usaidizi, lakini kisa kimoja jimbo la Ohio kimewashangaza wengi.
Polisi walipigiwa simu mapema Jumamosi na mwanamume aliyekuwa
anahangaishwa na nguruwe.
Polisi walidhani pengine mwanamume huyo alikuwa anaota au
alikuwa amelewa alipowaambia kwamba alikuwa anaandamwa na nguruwe akienda
nyumbani.
"Tulifika kwa mwanamume huyo tuliyedhani alikuwa mlevi na
kwamba alikuwa anaelekea nyumbani kutoka kwenye saa 11:26 asubuhi,"
polisi hao wanasema kwenye Facebook.
Lakini walipofika walimpata mwanamume alikuwa hajalewa hata
kidogo, lakini hakufurahia kabisa kufuatwa na nguruwe.
Alikuwa anafutwa na nguruwe lakini hakujua afanye nini, polisi
wa kituo cha Ridgeville Kaskazini wamesema.
Mwisho wa ujumbe wa Facebook wa North Ridgeville Police
Department
Polisi mmoja alifanikiwa kumkamata nguruwe huyo na kumuingiza
kwenye gari la polisi na kumpiga picha.
Nguruwe huyo pia alipelekwa kwenye seli (chumba cha kuwafugia
mbwa wa polisi) kabla ya kukabidhiwa kwa mmiliki wake Jumapili asubuhi.
Chanzo- BBC
No comments