MWENGE WA UHURU UMEWASILI MKOANI NJOMBE
Mwenge wa Uhuru umeshawasili Mkoani Njombe na kupokelewa asubuhi ya leo Mjini Makambako ukiwa umetokea Mkoani Iringa
Ukiwa Halmashauri ya Mji Makambako utakimbizwa kwa siku mbili(Leo na kesho)ambapo kesho kutwa tarehe 30 May 2018 Mwenge utapokelewa Wilayani Makete kata ya Mfumbi
Mwenge huo utakuwa Wilayani Makete kwa siku mbili kati ya Tarehe 30 na 31 May 2018 na kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo za kuzindua miradi na kuweka mawe ya Msingi kwenye miradi ya ujenzi na kuhamasisha shughuli mbalimbali za Kimaendeleo
Miradi ya bil 21imekaguliwa na kuzinduliwa mkoa wa Iringa huku Njombe miradi yenye thamani zaidi ya bil 5 kukaguliwa na kuzinduliwa
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu "ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA;WEKEZA SASA KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU"
No comments