Mwanafunzi
wa darasa la nne katika shule ya msingi Sabasaba jijini Mwanza, Dotto Baraka
(13) amefariki dunia baada ya kulipukiwa na betri ya simu aliyokuwa
akiunganisha na radio chakavu.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha tukio hilo ambapo amesema
limetokea Mei 17, mtaa wa Igoma Mashariki jijini Mwanza.
“Baada ya kutoka shuleni, marehemu akiwa na watoto wenzake alianza kutengeneza radio chakavu kwa kuchukua betri ya simu na kuunganisha kwenye nyanya za radio hiyo akitumia mdomo ndipo mlipuko ulipotokea na kusababisha kifo chake," amesema Kamanda Msangi.
Aidha
Kamanda Msangi ameongeza kuwa wakati tukio hilo linatokea, wazazi wa watoto hao
walikuwa safarini huko wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Hata hivyo katika tukio hilo hakuna mtoto
mwingine aliyejeruhiwa.
No comments