Header Ads

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI IPELELE WAELEZA CHANGAMOTO YA KUKOSA UMEME KWA ZAIDI YA MIEZI MITANO WILAYANI MAKETE

Image result for PICHA ZA UMEME

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ipelele iliyopo kata ya Ipelele Wilayani Makete Mkoani Njombe wamekosa huduma ya Umeme Takribani miezi mitano (5) kutokana na kuungua kwa Transfoma iliyokuwa ikitoa huduma hiyo shuleni hapo.

Mkuu wa shule ya sekondari Ipelele Mwalimu JOHN AMONI amesema tatizo la kutokuwepo kwa Umeme Shule ya Sekondari Ipelele kumepelekea kiwango cha Taaluma kwa Wanafunzi kushuka kutokana na kushidwa kupata muda wa ziada nyakati za usiku ili kujisomea zaidi.

Mwalimu JOHN AMONI amesema tatizo la kukosekana kwa huduma hiyo ni la muda mrefu tokea mwishoni mwa mwaka jana mpaka hivi sasa bado tatizo hilo halijapatiwa ufumbuzi pamoja na kuwasiliana na Meneja wa Tanseco Wilaya ya Makete mara kwa mara.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Ipelele wameliomba Shirika la Umeme TANESCO Wilaya ya Makete kuwasaidia kutatua changamoto hiyo huku wakisema kuwa changamoto wanazokumbana nazo wakati Umeme haupo  ni kutopata muda wa ziada wa kujisomea usiku ili kuongeza kiwango cha Taaluma.

Kitulo Radio fm imemtafuta Meneja wa Tanesko Wilaya ya Makete  Bw.RENATUSI MATINDE lengo ni kutaka kujua tatizo la  kukosekana kwa Huduma ya Umeme Shule ya Sekondari Ipelele amekiri kuwepo kwa tatizo hilo huku akisema kuwa tatizo ni kuungua kwa Transifoma na wanaendelea kushughulikia kuitafuta nyingine ili Wanafunzi waendelee kupata huduma hiyo.

No comments

Powered by Blogger.