MWENYEKITI UVCCM MKOA WA NJOMBE AGAWA MIPIRA KWA VIJANA WILAYANI MAKETE
Kutoka Kulia ni Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve akimkabidhi mipira hiyo Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Makete Ndg.Nehemia Sanga kwa niaba ya Vijana wa umoja huo
Mwenyekiti Umoja wa Vijana CCM(Uvccm) Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve amegawa mipira mitatu kwa Vijana Umoja wa Vijana wa Chama hicho Wilayani Makete Mkoani Njombe
Nehemia Tweve amesema mipira hiyo itawaongezea vijana uwezo wa kutambua umuhimu wa Michezo kwa kuwa michezo ni Afya lakini pia inawafanya vijana kubadilishana Mawazo yao ya kulijenga Taifa wanapokuwa Mazoezini kuliko kukaa vijiweni
Mwishoni mwa wiku iliyopita alikuwa Ziarani Wilayani Makete kwa lengo la kukutana na Vijana wa Chama hicho na kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na vijana hao huku akimtaka Mwenyekiti wa Umoja huo Wilaya ya Makete Ndg.Nehemia Kayanda Sanga kuandaa mpango wa kuwa na SACCOS ya Vijana Makete na apeleke Mpango huo ofisi za Umoja huo Mkoani tarehe 23 Mwezi huu
Wiki iliyopita Mwenyekiti wa umoja huo Mkoa Nehemia Tweve amefanya Ziara katika Wilaya zote za Mkoa wa Njombe na kukutana na Vijana mbalimbali huku akibadilishan nao Mawazo katika kukiimarisha chama chao
No comments