MBUNGE JIMBO LA MAKETE ATEKELEZA AHADI YAKE KWA VILABU VYA MPIRA WA MIGUU WILAYANI MAKETE
Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Vatcan Fc Abel Sheyo akipokea Jezi kutoka kwa Mwakilishi wa Mbunge Felix Kyando
Mbunge wa Jimbo la Makete Prof.Norman Sigalla King amekamilisha ahadi yake ya kutoa jezi kwa wachezaji wa Timu tatu zilizoshiriki Ligi ya Mkoa wa Njombe kutoka Jimboni kwake Makete.
Akikabidhi Jezi hizo kwa niaba ya Mbunge huyo Mwakilishi wake Felix Kyando amesema Mh.Mbunge ni mpenda michezo na Ahadi yake kwa WanaMakete ni Vitendo kwanza Maneno baadaye,hivyo yeye ameamua kufanya vitendo zaidi kuliko maneno.
Amesema timu ya Vatcan Fc ndio timu pekee ambayo haikupata Jezi alizogawa kati ya timu tatu zilizoshiriki Ligi ya Mkoa wa Njombe kutoka Wilayani Makete ambazo ni Kipagalo Fc na Usalama Fc
Akipokea Jezi hizo Mwakilishi wa Vilabu Wilayani Makete Conrad Mpila amemshukuru Mh.Mbunge kwa kutekeleza Ahadi yake na amemuomba kutosita kuendelea kuzisaidia timu mbalimbali na Vilabu vinavyotambulika Wilayani hapa
Pia amemuomba Mbunge kuona namna ya Kukarabati uwanja wa Wilaya unaotumika mara kwa mara kwa Mashindano ya Kata, Wilaya na hata Mkoa kwa kuwa uwanja huo unahitaji hadhi yake ambapo kwa sasa unakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kutokuwa na vyoo,uzio na miundombinu mingine
Abel Sheyo ni Mwenyekiti wa Klabu ya Vatcan Fc ya Makete Mjini amesema kuwa utekelezaji wa Ahadi hiyo unawafanya wapenzi wa Michezo Makete kuendelea kuongeza uaminifu kwa Mbunge na hususani upande wa kuinua michezo kwa Wilaya ya Makete
Felix Kyando mwakilishi wa Mbunge amesema Jezi hizo za Timu tatu(Kipagalo Fc,Vatcan Fc na Usalama Fc)zinagharimu kiasi cha Shilingi Milioni moja laki tatu na Elfu sitini(1,360,000)
No comments