WALIMU WAKUU SHULE 10 ZA MWISHO KUACHIA NGAZI LUDEWA-NJOMBE
Na Maiko Luoga
Mkuu Wa Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Mh, Andrea Tsere Amewataka
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari Ambao Shule zao Zimeshika
Nafasi za Mikia zilizopo Katika Makundi ya Shule Kumi Duni Kwa matokeo
ya Darasa la Saba na kidato cha Nne mwaka 2017 Wajiuzuru Nafasi zao za
Ukuu wa Shule kwa kuwa Wameshindwa Kutekeleza Majukumu yao.
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Ametoa Maagizo hayo February 20/2018 Kwenye
Mkutano wa Wadau wa Maendeleo Wilaya ya Ludewa Mkutano Uliofanyika
Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ukiwa na Lengo Kubwa la
Kujadili Kiwango cha Elimu Katika Wilaya ya Ludewa ambapo Shule za
Msingi na Sekondari za Wilaya ya Ludewa kwa miaka Mitano iliyopita
Zimekuwa zikifanya Vibaya Katika Matokeo yake na Kushika Nafasi za
Mwisho Kimkoa.
No comments