UHIFADHI MAZINGIRA NA VYANZO VYA MAJI NI MUHIMU SANA KWA ZIWA NYASA
Hii ni picha ikionyesha Ziwa Nyasa kwa mbali na Milima Livingston iliyopigwa Kijiji cha Ihanga kilichopo kata ya Ukwama
Na Furahisha Nundu
Elimu kuhusu Matumizi bora ya Ardhi na utunzaji wa Mazingira na
vyanzo vya Maji inaendelea kutolewa kwa Wananchi wa Makete Mkoani Njombe
ili kulinda Ziwa NyasaElimu hiyo imetolewa kwa Wananchi wa kijiji cha Kisasatu kilichopo kata ya Mbalatse,Ugabwa kata ya Lupalilo na Utengule Kata ya Kipagalo na Idara ya Mazingira na Misitu,Mwanasheria Halmashauri ya Wilaya na Idara ya Ardhi
Inaelezwa kuwa Maji ya Ziwa Nyasa yameanza kupungua kutokana na
Uharibifu wa Mazingira ambapo Mazingira yaliyoharibiwa ni Kutoka katika
Wilaya zinazotiririsha maji Katika Bonde la Nyasa Wilaya hiyo ni Makete,Ludewa,Rungwe,Ileje na Nyasa
No comments