Header Ads

MTOTO AUGUA ZAIDI YA MIAKA 10 UGONJWA USIOJULIKANA NJOMBE

Na Michael Mvelu Njombe

Serikali Mkoni Njombe imeombwa kutoa misaada kwa wahanga wanao ishi katika mazingira magumu na hatarishi ili kunusuru maisha  yao kwani wamekuwa wanashindwa kukidhi mahitaji muhimu katika familia zao ikiwemo chakula na malazi

Ni katika hali isiyo ya kawaida kwa mtoto James Ndelwa mwenye umri wa miaka 16 mkazi wa mtaa wa Kihesa Halmashauri ya Mji Njombe Mkoani Njombe amekuwa anasumbuliwa na ugojwa usio julika, huku vipimo kutoka kwa madaktari vikionesha kuto kuwepo kwa ugonjwa wowote kama anavo eleza Felister Sanga ambae ni mama mzazi wa mtoto huyo amesema kuwa zaidi ya miaka kumi mtoto wake huyo amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa Usiojulikana huku akiwa amezunguka kwenye vituo mbalimbali vya afya bila mafanikio yoyote

Majirani ambao wamekuwa wanamsaidi mama huyo katika kuhakikisha kwamba wanampa faraja na matumaini ya kuishi na mtoto huyo wameiomba jamii pamoja na serikali na asasi mbalimbali mkoani hapa kumpa msaada mama huyo ili kumwezesha mtoto huyo kupona kwani mama mzazi wa mtoto huyo amekuwa anashinda bila kufanya kazi inayo weza kumwingizia kipato kwa kushinda anamwangalia mtoto huyo.

Jesca Sanga ambaye ni Jirani na Mama James anasema "Kwa kweli huyu jirani yangu namunea huruma sana jinsi anavyonyanyasika na huyu mtoto ameteseka kwa siku nyingi sana,kwa sababu hata mama mwenyewe anashindwa hata kufanya kazi tunashindwa hata kuelewa huyu mtoto anatatizo gani yaani"

Fadhili Luvanda ni Msimamizi wa mashauri ya Watoto katika mtaa wa Kihesa Halmashauri ya Mji wa Njombe amesema kuwa mtoto huyo amegundulika kuwa ni mgonjwa mara baada ya kupita kila kaya kukutana na jamii ili kuwatambua watoto waishio katika mazingira hatarishi huku akitumia mwanya huo kuiomba jamii kuweza kumsaidia mama huyo.
 


No comments

Powered by Blogger.