MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WANAHABARI JUU YA MASWALA YA USAWA KIJINSIA YANAENDELEA MJINI DODOMA.
Waandishi wa habari kutoka
redio za jamii nchini wameendelea kujengewa uwezo juu ya maswala ya habari za
uchunguzi mafunzo yanayoendelea mjini Dodoma ndani ya ukumbi wa TBA
Wakitaja baadhi ya
changamoto zinazowakabiri waandishi hao katika utekelezaji wa majukumu yao
wawapo kazini ni kukosa ushirikiano kwa
vyanzo husika vya habari jambo ambalo hupelekea kucheleweshewa kukamilisha taarifa
kwa wakati.
Waandishi hao wakiwamo wa
kituo cha redio kutoka bunda wamesema kumekuwa na ugumu wa kutoa taarifa kwa
jamii kutokana na viongozi kutaka kutekeleza kero hizo pasipo kuripotiwa katika
vituo vya redio.
Nae mwandamizi wa mafunzo
hayo Bi.ROSE MWALIMU amewataka waandishi wa habari kufuata maadili ya kazi zao
ikiwa ni pamoja na kusikiliza matakwa ya vyanzo vyao vya habari ili kulinda
kazi zao pamoja na vituo vya redio kiujumla.
Tazama baaadhi ya picha za washiriki:-
Tazama baaadhi ya picha za washiriki:-
No comments