Wanawake waliovishana pete waachiwa kwa dhamana
Washtakiwa
wanne katika shauri la kufanya vitendo vinavyoashiria mapenzi ya jinsia
moja na makosa la kimtandao wameachiwa kwa dhamana baada ya Mahakama ya
Hakimu Mkazi Mwanza kutupilia mbali hoja za kuzuia dhamana zao
zilizowasilishwa na upande wa Jamhuri.
Uamuzi
huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Wilbert Chuma leo
Desemba 15, baada ya kukubaliana na hoja za mawakili wa utetezi, Mashaka
Tuguta, Ogastini Kulwa na Jebra Kambole kuwa hoja zilizowasilishwa na
upande wa mashtaka ni dhaifu mbele ya macho ya sheria.
Washtakiwa
katika shauri hilo namba 548/2017 ni Milembe Suleiman na Janeth Shonza
wanaodaiwa kuvishana pete ya uchumba licha ya wote kuwa wanawake.
Wengine
ni Aneth Mkuki anadaiwa kufanikisha sherehe wawili hao kuvishana pete
na Richard Fabian anayeshtakiwa kwa kosa la mtandao kwa kusambaza video
za tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii.
Katika
uamuzi wake, Hakimu Chuma amesema Mahakama haiwezi kufanyia kazi
maelezo na vitu vya mashaka na uvumi kuwa washtakiwa wanaweza kudhuriwa
na jamii iliyochukizwa na kitendo wanachoshtakiwa nacho.
“Ni
uamuzi wa Mahakama kuwa dhamana ni haki ya washtakiwa na upande wa
mashtaka umeshindwa kuwasilisha hoja za msingi kwa nini wanyimwe dhamana
zaidi ya kutoa hoja za hisia kuwa wakiachiwa watadhuriwa na jamii bila
kueleza watadhurikaje na nani haswa atawadhuru,” amesema Hakimu Chuma
katika uamuzi wake
No comments