Spika wa Bunge Aahidi Kwenda Nairobi Kumtembelea Tundu Lissu
Spika
wa Bunge, Mhe. Job Ndugai amefunguka na kusema atakwenda jijini
Nairobi nchini Kenya kumuona Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
ambaye anafanyiwa matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya
kufuatia kupigwa risasi Septemba 7, 2017.
Job
Ndugai amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
mjini Dodoma nyumbani kwake na kusema kuwa watakwenda kumuona Tundu
Lissu kwani ni mbunge wao na wao wanampenda sana na kudai kuwa kipindi
cha nyuma alishindwa kwenda Kenya kwa kuwa nchi hiyo ilikuwa kwenye
uchaguzi na haikuwa na utulivu wa kisiasa ila kwa kuwa saizi imetulia
anatarajia kwenda baada ya Christmas kumjulia hali.
"Mimi
kama Spika siwezi kwenda na kutoka navyotaka Kenya bali napokwenda kule
lazima kuwe na taarifa rasmi za kiserikali na kibunge na ninapokelewa
hivyo na ninapopelekwa huko hospitali au wapi napelekwa kwa utaratibu
huo ndiyo utaratibu wa nchi kwa nchi. Haiwezekani wao wana mechi kama
zile (Uchaguzi) halafu spika nazunguka zunguka Nairobi wanaweza kusema
ajenda aliyokuja nayo huyu siyo hii, katika pande hizi mbili Watanzania
wamemtuma huyu ana ajenda nyingine kwa hiyo unapokuwa kiongozi lazima
ujiongeze" alisema Spika Ndugai
Ndugai
aliendelea kueleza kuwa "Haukuwa wakati mzuri kwenda Nairobi, ila kwa
kuwa haya mambo yamepita na serikali saizi imekaa sawa sawa basi
tusubiri Christmas ipite baada ya hapo mtamuona Spika muda si mrefu
akienda kumuona Mbunge wake Nairobi au mahali pengine popote pale, yule
ni Mbunge wetu na tunampenda sana na tusingependa asikitike kwa lolote
lile" alimalizia Ndugai
Mbunge
Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi Septemba 7, 2017 akiwa mjini
Dodoma na baadaye kupelekwa nchini Kenya jijini Nairobi kwa matibabu
ambapo mpaka sasa yupo huko anaendelea na matibabu.
No comments