"Jambazi" amuua polisi kwa Kumpiga Risasi
POLISI mkoani Mara, Ephraim Lazaro (G- 1379), ameuawa kwa kupigwa risasi
na mtu anayedaiwa kuwa ni jambazi aliyekuwa ametoroka kutoka mahakamani zaidi ya mwezi mmoja uliopita na kufuatiliwa baada ya
kupata taarifa zake mahali alipokuwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jafar
Mohamed, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 7.00
mchana katika Kata ya Buruma wilayani Butiama ambako askari walikwenda
eneo hilo kumfuatilia mtuhumiwa.
Alisema askari wake alipigwa risasi na jambazi huyo aliyefahamika kwa jina la Mbogo James, maarufu kwa jina la China.
Alisema jambazi huyo alikamatwa akiwa na wenzake wawili.
Alisema mtuhumiwa alikuwa akitafutwa baada ya kutoroka mahakamani akiwa anakabiliwa na kesi ya mauaji na unyang’anyi wa
kutumia silaha iliyokuwa ikimkabili.
“Tulipata taarifa za mtuhumiwa huyu na askari wetu walikwenda kumfuatilia eneo husika.
No comments