WATUMISHI JIENDELEZENI KIELIMU HUSUSANI WALIMU:-ANTONY MPILUKA
Watumishi wa
Umma Wilayani Makete Mkoani Njombe wametakiwa kujiendeleza Kielimu ili kuendana
na Utendaji wa kisasa wenye kuzingatia Elimu na Teknolojia zaidi
Kutoka kulia ni Mwl.Mstaafu Jonick Ngogo aliyekuwa anaagwa,wa pili kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi H/w ya Makete Eliabu Simba na watatu kutoka kulia ni Mwl.Antony Mpiluka aliyekuwa anaagwa mara baada ya kustaafu wakiwa katika ukumbi wa Mikutano wa H/w Makete
Rai hiyo
imetolewa mwishoni mwa juma hili na Aliyekuwa Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Makete
Mwl.Antony Mpiluka akiwa katika hafla fupi ya kuagwa yeye pamoja na Mratibu
Elimu Tarafa ya Matamba Mwl.Jonick Ngogo baada ya muda wa Kustaafu utumishi wa
Umma kufika
Mwl.Antony
Mpiluka amesema suala la walimu na watumishi wengine kujiendeleza kielimu ni
jambo muhimu sana kwa Mazingira ya Ulimwengu wa Kisasa kulingana na umuhimu wa
Elimu inavyozidi kuboreshwa
Mwl.Antony
Mpiluka ameongeza kuwa ushirikiano kati ya watumishi ni muhimu katika kuboresha
utoaji na upatikanaji wa Huduma,pamoja na kustaafu ameahidi kuendelea kushirikiana na
watumishi akiwa kama Mzee mstaafu
Kwa upande
wake Mratibu Elimu Tarafa ya Matamba Mwl. Jonick Ngogo naye akiwa katika hafla hiyo ya kuagwa iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete amesema pamoja na kuwa
amestaafu lakini ataendelea kutambua mchango wake Serikalini na kuendelea kutoa
ushirikiano kwa watumishi wengine huku akiwashukuru watumishi wa Matamba na watumishi wengine waliokuwa wakishirikiana pamoja katika majukumu mbalimbali ya kijamii na kiserikali
Kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Makete Fransis Namaumbo,Ndg.Eliabu Simba
amewasihi wastaafu hao kuendelea kuishi maisha ya kumtumaini Mungu na
uwajibikaji ili kuendana na hali halisi ya Maisha ya uzeeni na kuishi vizuri na jamii inayowazunguka
Baadhi ya
Watumishi waliohudhuria hafla hiyo ya kumuaga Afisa Elimu Wilaya ya Makete
Mwl.Antony Mpiluka na Mratibu Elimu Tarafa ya Matamba Mwl. Jonick Ngogo
wamewamwagia sifa wastaafu hao kwa utumishi wao uliotukuka kazini na kuwaomba watumishi wengine kuiga mifano ya
wazee hao
Baadhi ya watumishi wakiwa katika ukumbi wa H/w Makete kwenye hafla ya kuwaaga Afisa Elimu Msingi Mwl.Antony Mpiluka na Mratibu Elimu Tarafa ya Matamba Mwl. Jonick Ngogo
Mwl.Antony Mpiluka aliyesimama akiwa katika majukumu yake kabla ya kustaafu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Makete Ndg.Fransic Namaumbo
Aliyekuwa Mratibu Elimu Tarafa ya Matamba Mwl. Jonick Ngogo mapema mwaka huu akikabidhiwa Zawadi na Bank ya NMB Tawi la Makete kwa kufaulisha vizuri wanafunzi shule za Msingi kwenye Tarafa yake
No comments