WALEVI SAA ZA KAZI WILAYANI MAKETE KUKIONA
Jeshi la Polisi Wilayani Makete limewataka
wananchi kuacha kunywa pombe kwa kupitiliza na kufuata muda wa kunywa pombe
kisheria ambao ni kuanzia saa 10 jioni
Akizungumza na Kitulo fm Afande peter Suwi
ambaye ni Operation officer Jeshi la polisi Wilaya ya Makete Mkoani Njombe amesema suala la
watu kuvunja Sheria na kunywa pombe muda usiokubalika wataendelea
kushughulikiwa kisheria kwa mujibu wa Sheria za nchi huku likitaja kijiji
mojawapo cha Ivalalila kilichopo kata ya Iwawa ambacho wananchi wake wamekuwa wakivunja sheria ya
unywaji wa Pombe
Jeshi hilo limesema kitendo cha watu kunywa
pombe kuanzia asubuhi ni uvunjaji wa Sheria na kitendo hicho kunasababisha
wananchi kushindwa kufanya shughuli za Maendeleo
"Sisi kama Jeshi la polisi tunataka watu wabadilike waache kunywa pombe saa za kazi na kuzingatia muda wa kuanza kunywa pombe haijalishi ni Klabu cha kuuza pombe za kinyeji au pombe kali"Aliongeza Afande Peter
Pia Jeshi hilo Wilayani hapa limesema
limejipanga vyema kuhakikisha Raia wake wanakuwa salama wakati wote wakifanya
kazi za Maendeleo na hivi sasa Kituo cha Tandala kimeongezewa Askari Polisi
pamoja na Gari jipya la Polisi limetolewa kwa ajili ya kuimarisha Ulinzi zaidi
Huku likijipanga kuweka kituo cha
Polisi Kidogo kata ya Kitulo kijiji cha Ujuni kulingana na Matukio mbalimbali
yanayotokea eneo hilo
"Tandala tumeongeza Askari Polisi wa kutosha lakini tumepeleka gari jipya kabisa pale kwa hivyo unaona ni namna gani vile tunataka Makete izidi kuwa salama,lakini pale ujuni kuna umuhimu mkubwa wa kuwepo kituo kidogo cha Polisi kulingana na mwingiliano mkubwa wa watu mbalimbali wanaoingia na kutoka kwa hiyo tupo kwenye mpango wa Haraka kufanya hivyo"Aliongeza
Kuhusu Kesi za Matukio ya Ubakaji na watu
wazima kushiriki kimapenzi na wanafunzi na kusababisha Mimba Jeshi hilo
limesema baadhi ya wazazi wanasababisha kesi hizo kutokuwa na nguvu na
kuachiliwa kwa watuhumiwa jambo ambalo limekuwa changamoto kubwa katika
utekelezaji wa sheria na kupambana na Mimba za utotoni
"Leo tu nilikuwa na Walimu wakuu wa Sekondari ya Lupila na Mang'oto kuhusu kesi hizohizo za wanafunzi (lakini hakutaja ni kesi gani)walimu wanalalamika kuhusu wazazi kumalizana na watuhumiwa majumbani kwao kwa hiyo inatuletea shida sana hii kuchukua sheria kwa watuhumiwa"
Sisi Polisi tunafurahi sana kuona mtu anahukumiwa kifungo hasa cha kwenda kutumikia jela lakini wazazi wanatuangusha pamoja na watoto wao,unakuta mtoto kituoni anatoa ushahidi vizuri tu lakini akifika Mahakamani anabadilisha alichokisema"
No comments