WADAU WA PAMBA WATOA MAAZIMIO
Wadau wa zao la pamba wametoa maazimio 10 ambayo wanasema yakitekelezwa yatasaidia kuinua sekta ya kutengeneza nguo nchini Tanzania.
Amesema wizara hiyo itaunda Kamati Maalumu itakayohusisha vijana wenye taaluma kutoka katika wizara hiyo ili kujifunza kutoka kwa wazee wazoefu waliopo katika sekta binafsi na hata kutembelea China kujifunza mifumo mbalimbali ukiwemo wa ulipaji kodi wa bidhaa zinazoingia nchini humo kutoka China.
Ole Gabriel amesema katika suala la uingizaji bidhaa za nguo hafifu kutoka nchi mbalimbali hasa China, taasisi zinazohusika na udhibiti ikiwemo Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na nyingine zilizopo nchini humo zinatakiwa kusimamia na kuhakikisha kwamba bidhaa hafifu na zilizo chini ya kiwango haziingii katika soko la Tanzania.
No comments