DEREVA BODABODA AFARIKI KWA KUGONGWA NA GARI KIJIJI CHA MFUMBI WILAYANI MAKETE
Kamanda Renatha Mzinga
Mtu mmoja
aliyetambulika kwa majina ya Faustin Joseph (50) Mkazi wa Chimala Mkoani Mbeya
amefariki Dunia kwa ajali ya kugongwa na gari akiwa anaendesha
Pikipiki(Bodaboda) Kijiji cha Mfumbi kata ya Mfumbi Wilayani Makete Mkoani
Njombe
Ajali hiyo
imetokea tarehe 20 May 2018 katika kijiji cha Mfumbi Wilayani Makete wakati
Dereva Erasto Yona(34) mkazi wa Kimara Dar es salaam akiendesha Gari lenye
namba T342 DLV aina ya Toyota ikiwa imetokea Kyela kuelekea Dar es salaam
aligonga pikipiki namba T825 CAY aina ya Skaymark iliyokuwa ikiendeshwa na
Dereva Faustin Joseph na kusababisha
kifo chake papo hapo na kujeruhi abiria wawili ambao ni Neema Bonifasi na Given
Faustin Melele
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Renatha Mzinga ametoa
taarifa hiyo na kuthibitisha kifo cha Dereva bodaboda huyo
Kamanda
Mzinga amesema Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe uliosababishwa na Dereva
bodaboda aliyekuwa akiingia Barabara kuu ya Mbeya-Dar bila kuchukua tahadhari
Kamanda
Mzinga amewataka Madereva Mkoani Njombe pindi waendeshapo vyombo vya Moto
barabarani kuchukua tahadhari na kuendesha vyombo hivyo kwa umakini na
kuzingatia taratibu na sheria za usalama Barabarani ili kuepuka ajali na
kusababisha vifo kwa watu wasio na hatia
Huku Jeshi
hilo la Polisi Mkoani Njombe likiongeza kwamba litaendelea kutoa Elimu ya
Usalama Barabarani kwa wananchi wote na kuwataka wananchi kuwa makini
wanapokuwa wanatembea kwa miguu barabarani
No comments