Header Ads

MBUNGE JIMBO LA MAKETE PROF.NORMAN SIGALA KING AKABIDHI AMBULANCE KITUO CHA AFYA

 Mwonekano wa gari hilo la kubeba wagonjwa kwa ndani

 Mbunge wa Jimbo la Makete Prof.Norman Sigala King akiwasha gari hiyo kama ishara ya kuonyesha kwamba gari inauwezo wa kubeba wagonjwa
 

Prof.Norman Sigala King Mbunge Jimbo la Makete Kushoto akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati Kituo cha afya Lupila Mwinjilisti JOMNAS GWATA(wa kwanza Kulia) na kummsihi Kwamba kamati hiyo ikalisimamie gari hilo kwa umakini ili liweze kutoa huduma stahiki wa wananchi hususani Akinamama wajawazito na wagonjwa wanaohitaji huduma za dharula

Mbunge Jimbo la Makete Profesa Norman Sigala King amekabidhi gari la kubeba wagonjwa Kituo cha Afya Lupila kilichopo Kata ya Lupila Tarafa ya Ukwama Wilayani Makete Mkoani Njombe

Mh.Prof.NORMANI SIGALA amekabidhi gari hilo mapema hii leo katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Makete na kusema kwamba kwa niaba ya Wananchi wa Makete amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta JOHN POMBE MAGUFULI kwa kuwaletea wananchi wa Lupila  gari la kubeba Wangonjwa(AMBULENCE)ambayo itawasaidia sana kinamama wajawazito

Vilevile Mh.Prof.Norman Sigala King amewataka wananchi wa Kata ya Lupila kulitunza gari hilo na kulihudumia ili liweze kudumu kwa muda mrefu na liwasaidie hasa wananchi wa Kata ya Lupila

Mwenyekiti wa kamati Kituo cha Afya Lupila  Mwinjilisti JOMNAS GWATA ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwaona wananchi wa Lupila na kuwapatia gari la kubeba wagonjwa pamoja na kwamba watapata  changamoto wakati wa masika lakini wanaamini kipindi cha kiangazi gari hilo litawasaidia 

Kwa upande wake Kaimu Mgaga Kituo cha Afya Lupila SALUMINA DONADI SALY ameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Makete pamoja na Serikali kwa kuchagua Kituo cha Afya Lupila kupata gari la kubeba Wagonjwa kwani wananchi wa Lupila wameteseka kwa muda mrefu hasa kwa kinamama wajawazito kwa kusafiri zaidi ya Km 40 kufuata huduma za Dharula Hospitali ya Mission Ikonda.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Makete Daktari  ITIKIJA MSUYA ameishukuru Serikali kwa ujumla wake na Mbunge wa Jimbo la Makete kwa kukabidhi gari hilo katika kamati inayoendesha kituo cha Afya Lupila.





1 comment:

Powered by Blogger.