Header Ads

WAANDISHI WA HABARI REDIO ZA JAMII TANZANIA WAENDELEA NA MAFUNZO MJINI DODOMA



Waandishi wa habari wa radio za Kijamii nchini Tanzania wametakiwa kuzingatia maadili ya taaluma zao ili kuandika habari zenye weledi katika kuzisaidia jamii zinazowazunguka.
Wito huo umetolewa leo mjini Dodoma na Mkufunzi wa musuala ya habari kutoka shirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni(UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu kwenye mafunzo ya siku nane yanayoendelea kwenye ukumbi  wa wakala wa majengo (TBA).
Bi. Rose amesema ili jamii inufaike na uwepo wa radio za Kijamii, waandishi wa habari wanatakiwa kuzingatia miiko na misingi inayowaongoza katika Kutekeleza majukumu yao  kwa manufaa ya umma na wao binafsi.
Kwa upande wao waandishi wa habari wa radio za kijamii wamelishukuru shirika la UNESCO na kuongeza kuwa mafunzo hayo yatawasidia katika kuboresha utendaji wao wa kazi katika vituo vyao.
Shirika la unesco linaeendelea kutoa mafunzo ya uandishi wa habari kwa radio za kijamii nchini  ili kuwajengea uwezo wa kuandaa habari na vipindi vyenye ubora.

tazama picha za washiriki:-

 









No comments

Powered by Blogger.