Waziri avutiwa na DC, Ammwagia sifa Kibao
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina amesifu utendaji kazi wa Mkuu wa
Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Godwin Gondwe katika usimamizi wenye
weledi wa sheria za mifugo nchini
Luhaga
ametoa sifa hizo kwa Gondwe akiwa kwenye ziara yake wilayani Handeni
ambapo amekemea tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali katika Hifadhi
za Misitu, Mapori ya Akiba na Serikali za Mitaa kukamata mifugo kiholela
na kutoza faini zisizo na misingi ya kisheria.
“Ninamsifu
mkuu wa Wilaya ya Handeni Ndugu Godwin Gondwe kwa utendaji wake mzuri
na ripoti ya mifugo wilayani kwake ni nzuri lakini watendaji wa Serikali
waliofanya hujuma na dhuluma kwa wafugaji hawatabaki salama,
tutawafuatilia na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria” amesema
Luhaga.
Waziri
Mpina ameongeza kuwa jumla ya kaya milioni 4.49 za kilimo nchini
zinajishughulisha na ufugaji mifugo ya aina mbalimbali. Pia ameweka wazi
kuwa kama sekta hiyo isingekuwa inazalisha mazao ya mifugo na Serikali
kuamua kuagiza kutoka nje ya nchi basi ingelazimu kutumia kiasi cha sh.
Trilioni 17.8.
Kwa
upande wake Godwin Gondwe amesema pamoja na pongezi za Waziri Mpina,
wao kama serikali ya Wilaya wataendelea kubuni mbinu mbalimbali za
kuboresha sekta ya ufugaji ikiwemo uimarishaji wa majosho, malisho na
uzuiaji uuzaji nyama kiholela barabarani.
No comments