Header Ads

Watiwa Mbaroni kwa kukutwa na dawa za kulevya

Kamanda wa Polisi Mkoa wa  Singida Debora Magiligimba  amesema Jeshi la Polisi Mkoani kwake linawashikilia watu  watatu kwa tuhuma  za kukutwa na madawa ya kulevya

Kamanda  Magiligimba amesema katika oparesheni ya kupambana na dawa za kulevya wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa na misokoto ya  bangi 238 sawa na gramu 484 na kete 80 za Heroin sawa na gramu 160.
Mbinu zilizotumika kuhifadhi  Heroin ni mtuhumiwa aliamua kuficha kete kwenye matundu ya sabufa na kuanza  kuuza kidogo kidogo na misokoto ya bangi ilifichwa kwenye begi dogo la nguo na kupuliziwa marashi ili kuzia harufu ya bangi.”,amesema Kamanda Magiligimba.
Kamanda Magiligimba amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baaada ya upelelezi kukamilika.

No comments

Powered by Blogger.