Header Ads

MWENGE WA UHURU KUKIMBIZWA TAREHE 30 NA 31 MAY WILAYANI MAKETE MKOANI NJOMBE

Image result for mwenge wa uhuru

Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa Wilayani Makete Mkoani Njombe Tarehe 30 May 2018 na kufanya shughuli mbalimbali za uzinduzi na kuweka mawe ya Msingi katika Miradi ya Maendeleo

Taarifa iliyotolewa na Mratibu wa Mbio za Mwenge Kiwilaya ambaye pia ni Afisa Vijana Wilaya Ndg.Bruno Mwangwale mbele ya Baraza la Madiwani Wilaya ya Makete hii leo amesema mwenge wa Uhuru utakuwa Makete kwa siku mbili kuanzia tarehe 30 na 31 May 2018 


Mratibu wa Mbio za Mwenge Kiwilaya Ndg.Bruno Mwangwale amesema Mwenge huo utapokelewa Kijiji cha Mfumbi Kata ya Mfumbi siku yaTarehe 30 mwezi wa Tano na mwenge huo utakesha Kijiji na Kata ya Tandala na tarehe 31 kukabidhiwa Wilaya ya Njombe

Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Makete utakimbizwa kutoka  kata ya Mfumbi kuelekea kata za Matamba,Mlondwe,Kitulo,Isapulano,Iwawa,Lupalilo na Mwisho Mwenge huo utakesha Kijiji na Kata ya Tandala

No comments

Powered by Blogger.