Header Ads

HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI

Image result for francis Namaumbo


Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete Ndg.Francis Namaumbo

Halmashauri ya Wilaya ya Makete Mkoani Njombe imepongezwa kwa kupata hati safi kwa mwaka wa Fedha 2016/17 kufuatia ukaguzi wa Mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu za Serikali

Pongezi hizo zimetolewa hapo jana na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete kwa Mkurugenzi Mtendaji na watendaji wake wote kwa kuongeza ufanisi katika uwajibikaji na kuipa Halmashauri sifa nzuri ya kutokuwa na hati ya Mashaka au hati chafu

Akitoa Taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu za Serikali Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Edward Mdagachule kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Makete Francis Namaumbo mbele ya Waheshimiwa Madiwani katika kikao cha Barala la Madiwani hapo jana kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri amesema Wilaya ya Makete kwa mwaka wa fedha 2016/17 imefanikiwa kupata hati safi

Waheshimiwa Madiwani wametumia nafasi hiyo kuipongeza Ofisi y Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Makete kwa utendaji kazi mzuri pamoja na watumishi wengine walioshiriki katika kuifanya Halmashauri ya Wilaya ya Makete kupata hati safi

Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Makete Mh.Jison Mbalizi ametoa rai kwa Waheshimiwa Madiwani,Watendaji na ofisi nzima ya Mkurugenzi kuendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali ya utendaji katika kuhakikisha hati hii inakuwa na Mwendelezo na siyo kuachiana majukumu au kuhujumiana kwenye kazi mbalimbali

No comments

Powered by Blogger.