Header Ads

MBUNGE PROF.NORMAN SIGALLA KING ASEMA MAISHA YA MTAANI NI TOFAUTI NA MAISHA YA DARASANI-IWAWA SEC

Mbunge wa Jimbo la Makete Prof.Norman Sigalla King amewataka Vijana wasomi kuacha kubagua kazi kwa kutofautisha Elimu zao na Maisha ya Mtaani kwa kuwa Maisha ya Mtaani yanahitaji kujiongeza na siyo Elimu ya Darasani pekee

Rai hiyo ameitoa Leo Ijumaa akiwa shule ya Sekondari Iwawa alipohudhuria mahafali ya Kidato cha sita kama Mgeni rasmi

Prof.Norman amesema Vijana wengi wanaohitimu Elimu za juu wamekuwa wakilalamika kukosa ajira ni kwa sababu ya kuchagua kazi kulingana na Elimu walizonazo bila kutambua kuwa Maisha ya Mtaani yanahitaji pia nyongeza ya Elimu ya Mtaani 

Pia amewataka wanafunzi wanaohitimu masomo yao mwaka huu Iwawa Sekondari kuishi kulingana na Mabadiliko ya Maisha bila kuishi Maisha ya Wengine


Mkuu wa shule ya Sekondari Shule ya Sekondari Iwawa Mwl.Fadhili Dononda amesema shule hiyo imekuwa ikionyesha mabadiliko mazuri kila mwaka upande wa Taaluma kwa kuwa hapo mwaka jana shule hiyo ilishika nafasi ya kwanza kimkoa,huku akiwapongeza walimu wa shule hiyo pamoja na wazazi kwa ushirikiano na umoja walionao

Wakati huo huo amewapongeza wanafunzi wa Kidato cha sita wanaohitimu na kuwataka kwenda kuwa mabalozi wazuri wa shule hiyo huko waendako


Diwani wa Kata ya Iwawa Mh.Asifiwe Luvanda akiwa katika Mahafali hayo amemshukuru Mh.Mbunge wa Jimbo la Makete Prof.Norman Sigalla kwa kuisaidia shule hiyo katika Nyanja mbalimbali na kuelezea mipango mikakati waliyonayo wazazi katika kuboresha Mazingira ya kujisomea wanafunzi waliopo shuleni hapo

Kwa upande wa wanafunzi wanaohitimu masomo yao wametoa ujumbe wa upendo kwa wanafunzi wanaoendelea na Masomo shuleni hapo kupitia Shairi waliloimba kuashiria walitamani kuendelea na Masomo shuleni hapo lakini Mpango wa Wizara unawataka kuhitimu kwa kipindi cha muda huo na kuwataka kuwa watiifu kwa walimu wao

Picha mbalimbali za Mahafali hayo tazama hapa chini
















No comments

Powered by Blogger.