Header Ads

MTOTO ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUDUMBUKIZWA KWENYE SHIMO LA CHOO MAKETE-NJOMBE




Mtoto wa umri wa miaka (13) anusurika kifo baada ya kutumbukizwa kwenye shimo la choo lenye urefu wa mita 24,kuokoa uhai wa mnyama (mbuzi) kwa ujira wa Tsh.1000/=(elfu moja ) na soda moja tukio lililotokea hivi karini katika kijiji cha bulongwa kilichopo kata ya bulongwa  wilayani makete mkoani njombe .

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa kitongoji cha lupaso bw,VELEHIM NAHOLI SANGA,amekili kutokea kwa tukio hilo kwenye kitongoji chake huku akitoa onyo kwa wananchi  kuondokana na vitendo vya kikatili dhidi ya watoto.

Wakiwa kwenye mkutano wa kitongoji cha Lupaso  baadhi ya wanchi wa kijiji cha bulongwa  wamasema tukio hilo limetokea siku ya Jumamosi mnamo tarehe 25/11/2017 majira ya mchana ambapo Bi, Huruma John Mahenge alifanya tukio hilo la kikatili dhidi ya mtoto mwenye  umri  wa miaka (13) anaye soma darasa la tano (5) katika shule ya msingi Bulongwa lakumshawaishi  na kumtumia motto huyo kuokoa uhai wa mbuzi aliye tumbukia kwenye choo kinachotumika kwa kumfunga kamba aina aya manira  kiunoni  mtoto huyo jamabo ambalo nikinyume cha sheria ya mtoto  no 21 ya mwaka 2009.

Twingitsiwe Mahenge ni bibi mlezi wa mtoto amesema mtoto huyo alifanyiwa kitendo hicho siku ya jumamosi ambapo yeye siku hiyo hakuwepo nyumbani na mara baada ya kurudi alibaini kudhoofu kwa mtoto huyo jambo lililompelekea  kumuuliza na kubaini kuwa mjukuu wake amefanyiwa ukatili hivyo alichukue hatua ya kutoa taarifa kwa viongozi wa kitongoji ili kupata msaada zaidi

Kwaupande wa mtoto aliyefanyiwa ukatili amesimlia jinsi alivofanyiwa kitendo hicho huku akieleza jinsi tendo hilo lilivyo muathili kiafya na kwamba alilazimishwa kufanya tukio hilo na alipo jaribu kukataa alitishiwa kuwa chapwa na shangazi yake ambaye nimhusika wa tukio hilo.

Waandishi wa habari walipofanya mahojiano na mhusika watukio hilo aliyetambulika kwajina  la HURUMA JOHN MAHENGE amekili kufanya tukio hilo huku akieleza kuwa alifanya kitendo hicho pasipo kujua kama ni kosa  kwa muujibu wa sheri na baadaya kugundua kuwa nikosa aliwaomba radhi ndugu huku akilili kumpekeka mtoto hospitari kwaajili ya vipimo ambapo daktari wazam alimpokea pasipo PF3 na kumpa dawa za maumivu na za mafua tu

Afisa mtendaji wakata ya bulongwa  bw, YUSTI KONGA, ametoa wito kwa jamii kutambua utu na thamani ya binadama kwa kutofanya ukatili dhidi ya watoto kwakuwa  watoto wana stili kupata haki zao za msingi kama binadam wengine pia amesema hatua na sheria itafuata mkondo wake ili iwefundisho na wawengine.

Bi,mary  Mnubi niafia ustawi wa jamii ngazi ya (w) ambaye  amesema wamepokea taarifa hiyo ingawa amesema taratibu za kufuatilia tukio hilo zina endelea na endapo zitakamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mhusika huku akisem vitendo vyakikatili dhidi ya mtoto  havikubliki katika jamii 

Kamanda wa pilisi (W) ya makete  OCD – OPTATUSI MAGANGA amekili kupokea taarifa hizo nakusema kwamba  uchunguzi wa tukio hilo unaendelea  na hatua za kisheria zitachukuliwa ili kuwa fundisho kwajamii nzima.

Juhudi za kumpata daktari aliye mfanyia uchunguzi mototo huyo bado zinaendelea.




No comments

Powered by Blogger.