Header Ads

MAKUBALIANO YA WALIMU NA DED UHAMISHO WA WALIMU KUTOKA SHULE ZA SEKONDARI KWENDA SHULE ZA MSINGI WILAYANI MAKETE HAYA HAPA


Walimu waliotakiwa kuhamishwa kutoka Shule za Sekondari kwenda Shule ya Msingi Wilayani Makete Mkoani Njombe baadhi yao wamerudi kufundidha Shule za Sekondari wakati wakisubiri Malipo ya Fedha za uhamisho
Kaimu Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Makete Mwl.Leopold Mlowe akizungumza kwenye Baraza la Madiwani lililofanyika hii leo Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete na ameelezea kuhusu uhamisho wa Walimu 

Kaimu Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Makete Mwl.Leopold Mlowe ameyasema hayo jioni ya leo akiwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Makete akielezea sababu za walimu hao kushindwa kuhamishwa kwenda shule za Msingi walikopangiwa

''Walimu waliokuwa wamechaguliwa kwenda kuongeza nguvu na kuziba pengo la upungufu wa walimu shule za Msingi waligoma kufanya kazi kwenye vituo walivyopangiwa na walichukua hatua ya kuja ofisi ya Mkurugenzi kudai malipo ya uhamisho ndipo waende kwenye shule walizopangiwa''

Mwl.Mlowe ameongeza kuwa''Baada ya kuja tulikaa na kukubaliana kwamba Halmashauri haina fedha za kuwalipa wao kama fedha za uhamisho na tukakubaliana wale wanaotaka kufundisha shule walizopangiwa wakafundishe na baadhi walikubali huku wengine wakikataa na tukakubaliana warudi kwenye shule walizokuwa ili tukipata fedha tutawalipa wote ili waende kwenye vituo vipya vya kazi''

Wakati huo huo Mlowe amewataka wananchi na Waheshimiwa Madiwani kuwa wavumilivu kuhusu changamoto ya upungufu mkubwa wa walimu kwa kuwa suala hilo linatambuliwa pia na Serikali na liko katika ngazi za kushughulikiwa ili kukabiliana na changamoto hiyo


Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakiwa kwenye kikao cha kujadili taarifa mbalimbali za kata wamehoji kuhusu walimu waliotakiwa kuhamishwa kutoka Shule za Sekondari kwenda Shule za Msingi zoezi hilo kushindwa kufanikiwa ndipo walipopatiwa majibu hayo na kutakiwa kuwa na subira katika jambo hilo


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Mh.Egnatio Mtawa amepongeza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Idara ya Elimu Msingi na Sekondari pamoja na Jitihada za Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg.Francis Namaumbo kwa maridhiano ya Amani na Maelewano baina yao na Walimu hao

Mh.Egnatio Mtawa amesema "tumesikia na kuona katika baadhi ya maeneo mengine walimu wameandamana na wengine kupoteza kazi lakini hayo mambo kwetu hayaleta athari kufuatia umakini wenu ninyi watendaji,Hongereni sana"

Kulia ni Makamu Mwenyekiti Halmahauri ya Wilaya ya Makete ambaye pia ni Diwani wa kata ya Iniho Mh.Josony Mbalizi,Katikati ni Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Makete ambaye pia ni Diwani kata ya Tandala Mh.Egnatio Mtawa na Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete Ndg.Francis Namaumbo wakiwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani jioni ya leo

No comments

Powered by Blogger.