Header Ads

"Jambazi" amuua polisi kwa Kumpiga Risasi

POLISI mkoani Mara, Ephraim Lazaro (G- 1379), ameuawa kwa kupigwa risasi na mtu anayedaiwa kuwa ni jambazi aliyekuwa ametoroka kutoka mahakamani zaidi ya mwezi mmoja uliopita na kufuatiliwa baada ya kupata taarifa zake mahali alipokuwa. 

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jafar Mohamed, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 7.00 mchana katika Kata ya Buruma wilayani Butiama ambako askari walikwenda eneo hilo kumfuatilia mtuhumiwa. 

Alisema askari wake alipigwa risasi na jambazi huyo aliyefahamika kwa jina la Mbogo James, maarufu kwa jina la China. Alisema jambazi huyo alikamatwa akiwa na wenzake wawili. 

Alisema mtuhumiwa alikuwa akitafutwa baada ya kutoroka mahakamani akiwa anakabiliwa na kesi ya mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha iliyokuwa ikimkabili. “Tulipata taarifa za mtuhumiwa huyu na askari wetu walikwenda kumfuatilia eneo husika. 

“Kwa bahati mbaya kabla hawajamfikia kumkamata alikuwa na silaha na alifyatua na kumpata askari wetu ambaye alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini.

No comments

Powered by Blogger.