Header Ads

KIJANA WA MIAKA 24 AJINYONGA MPAKA KUFA MSITUNI KIJIJI CHA IVALALILA WILAYANI MAKETE




Image may contain: tree, plant, outdoor and natureKijana Jastini Ilomo (24) mkazi wa kijiji cha Ivalalila kata ya Iwawa Wilayani Makete amejinyonga mpaka kufa kwa kutumia Kamba akiwa kwenye shamba lake la miti ya mbao
Kijana huyo inasadikika alipotea nyumbani tokea jumapili usiku wa kuamkia Jana jumatatu na alikuwa akiishi peke yake baada ya kuachana na mkewe siku chache zilizopita
Haijajulikana sababu ya kujinyonya kwake kutokana na kutokuwepo viashiria vyovyote vya yeye kuamua kuchukua maamuzi hayo,Mwili wake umegundulika hapo jana na kina mama waliokuwa wakisomba mbao msituni takribani kilomita 3 kutoka kijijini hapo

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kikusi Emmanuel Ilomo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kwamba Marehemu alipotea katika mazingira yasiyoeleweka siku ya Jumapili usiku au jumatau asubuhi na jana Jumanne ndipo wakagundua kuwa amenjinyonga Msituni


Wananachi wa kijiji hicho akiwemo Baba Mkubwa wa Marehemu wameelezea masikitiko yao kufuatia tukio hilo huku wakitoa wito kwa wananchi kutochukua maamuzi yanayoweza kuhatarisha uhai wao badala yake watafute mbadala wa kutatua tatizo

Kaka wa Marehemu Nickolaus Ilomo anasema Mdogo wake hakuwa na tatizo lolote lakini hajui ni nini kilichomtokea Mdogo wake mpaka kuchukua maamuzi hayo

Mwili wa Marehemu umezikwa jana,MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI ALIPOPACHAGUA ENZI ZA UHAI WAKE AMINA.

No comments

Powered by Blogger.