Header Ads

CHAMA CHA MAENDELEO MAKETE(MDA) KITAIJENGA MAKETE MPYA


Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh.Veronica Kessy amwaga pongezi nyingi kwa wadau wa Maendeleo Wilayani Makete kwa Umoja wao na Ushirikiano walionao katika kuijenga Wilaya yao ya Makete

Pongezi hizo zimetolewa mapema hapo jana wakati wa Makabidhiano ya Vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Wadau wa Chama cha Maendeleo Makete (MDA) kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Bweni la Wavulana shule ya Sekondari Mang’oto lililoteketea kwa moto usiku wa tarehe 12 March 2018 na kutekeleteza vitu mbalimbali vilivyokuwa na thamani ya zaidi ya shilingi Milioni tisini pamoja na Bweni

Mh.Veronica Kessy amesema “sambamba na Kauli mbiu ya Chama hicho ya Pamoja tuijenge Makete kwa ushirikiano huu lazima Makete itajengeka haswa”

“Nimekuwa nikiona harakati Mnazozifanya (MDA) kwa Umoja wenu najua ninyi ni wawakilishi tu wa wengi waliopo kwenye Umoja huo lakini sina budi kutoa pongezi zangu za dhati kwa moyo mlionao wa kujitoa kwa hali na mali katika kuhakikisha mnarudi kwenu na kuwekeza,Mungu yuko pamoja nanyi na ninaimani kuwa mtawekeza kweli kweli”

“Pia kwa sababu nyinyi MDA mmenifanyia surprise na mimi nawafanyia surprise vilevile Hili Jengo linalojengwa kwa ajili ya Bweni la wavulana likikamilika litapewa jina la MDA”

“Sasahivi tunafursa ya ujenzi wa Barabara ya kiwango cha Lami kutoka Njombe-Makete nadhani mmeona wakandarasi wanavyochakalika kwa hiyo Makete itafunguka na kuwa kisiwa cha ukuzaji wa Uchumi siyo Makete tu hata katika Mkoa wetu wa Njombe,kwa hiyo waambieni na wengine waje waanze kuwekeza Makete hususani katika upande wa Kilimo cha Matunda Mbalimbali kama Parachichi,apple na Matunda mbalimbali,Mazao ya Viazi na mazao mengine mengi ambayo kwa ardhi ya Makete aliyoijalia Mungu Neema ya kila zao kustawi hii ni Fursa kubwa sana kwetu wanaMakete na wana MDA popote mlipo nasema karibuni sana”Aliongeza Mkuu huyo wa Wilaya

Makamu Mwenyekiti wa MDA Ndg.Philipo Mahenge akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Makete vifaa hivyo katika taarifa yake amesema “Mh.Mkuu wetu wa Wilaya Vifaa hivi ni kutokana na Michango ya wadau mbalimbali ambao ni wazawa wa Makete na ambao siyo wanaMakete lakini wenye Mapenzi mema na Makete wameamua kuchanga fedha na kununua vifaa vifuatavyo:-Mifuko 100 ya Saruji,Bati 150 na Misumari ya bati Kilo 10 kwa lengo la kuhakikisha watoto wetu,wadogo zetu wanapata mahala pazuri pa kulala ili waweze kusoma katika Mazingira ya kuvutia”

“Pamoja na jitihada hizi sisi kama MDA tunatoa pole kwa wote walioathirika na Janga hili la moto,MDA inalengo la kuwaunganisha wanaMakete waishio ndani ya Wilaya na Nje ya Wilaya katika Nyanja mbalimbali Kiuchumi na MDA siyo chama cha kisiasa”Aliongeza Ndg.Philipo Mahenge

Philipo Mahenge aliongeza kuwa “Katika Umoja wetu tuliamua kukusanya Michango mbalimbali kutoka kwa wadau na tumepata mwitikio mkubwa na waliochangia ni kutoka kwa wadau wenyewe,Makampuni Mbalimbali yanayomilikiwa na wanaMakete na Kampuni moja ya Kihindi imetuchangia pia,wanafunzi wenye asili ya Makete wanaosoma vyuo vikuu wamejikusanya na kuchangia baada ya hapo michango yao wakaiwasilisha kwenye umoja huu na wadau wengine wasio wanaMakete wenye Mapenzi mema na Wilaya ya Makete”

“Mh.Mkuu wa Wilaya tunawapongeza wananchi wote wa kata ya Mang’oto na Wilaya yote kwa ujumla kwa hatua muhimu ambazo mmezichukua katika kuwasaidia wanafunzi ambao wamepatwa na janga la moto,tunawapongeza pia kwa hatua ya Ujenzi ambayo inaendelea na sisi kama MDA tunaongeza nguvu na kuwapa ushirikiano pale mlipofikia na ikiwezekana ushirikiano mwingine utaendelea kuwepo huko mbeleni Hongereni sana”Aliongeza

Unaweza kutizama picha Mbalimbali za tukio hilo hapa chini
 Kutoka kushoto ni Naibu katibu wa Chama cha Maendeleo Makete(MDA) Monny Luvanda,Makamu mwenyekiti wa MDA Ndg.Philipo Mahenge,Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh.Veronica Kessy na wa Mwisho kulia ni Mkuu wa shule ya Sekondari Mang’oto Bonavetura Mgaya ambaye anaelezea hatua ambayo imefikiwa sasa katika ujenzi wa Bweni hilo


Hili ni Jengo linalojendelea kujengwa ambalo limefikia hatua ya Lenta kwa muda wa wiki mbili
Katika Picha ni Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh.Veronica Kessy mwenye koti jeusi akiwa na Viongozi wa MDA na viongozi kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Makete
Picha ni Ujenzi wa Bweni ukiendelea na huo ni mwonekano wake kwa mbele

Mkuu wa shule ya Sekondari Mang’oto Bonavetura Mgaya akielezea Jambo kuhusu shule hiyo ya Sekondari Mang’oto na kuongeza kuwa kwa sasa wanafunzi zaidi ya mia moja bado wanalala kwenye vyumba vya Madarasa

Viongozi wa Cahama cha Maendeleo Makete(MDA) kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa MDA Ndg.Philipo Mahenge,katikati ni Katibu wa Chama hicho Bw.Award Mpandila na kushoto kwake ni Naibu Katibu wa Chama hicho Bi.Monny Luvanda wakiwa kwenye Makabidhiano ya Vifaa hivyo na kusikiliza taarifa ya Maendeleo ya Ujenzi wa Bweni hilo na mahali ulipofikia iliyokuwa ikisomwa na Afisa Mtendaji kata ya Mang’oto Bw.Mengi Chalamila

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mang’oto waliofika shuleni hapo kuhudhuria makabidhiano ya vifaa hivyo

Wanafunzi wa shule ya sekondari Mang’oto wakiwasikiliza wageni waliofika shuleni hapo kukabidhi vifaa hivyo

Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Makete Mwl.Jacob Meena akitoa neon la shukrani kwa wana MDA kwa  niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete

Bi.Monny Luvanda Naibu Katibu wa MDA akitoa Salamu za wanaMDA katika Mkusanyiko wa watu mbalimbali waliokuwepo shuleni hapo

Katibu wa MDA Bw.Award Mpandila akitolea Maelezo namna ya kujiunga na MDA ili uwe Mwanachama na Mkononi akiwa ameshika Katiba ya Chama hicho ambayo baadaye alimkabidhi Mkuu wa Shule ya Mang’oto Sekondari ili naye aisome

Award Mpandila akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari Katiba ya Chama hicho (MDA)

Makamu mwenyekiti wa MDA Ndg.Philipo Mahenge akizungumza na wananchi wa Kata ya Mang’oto pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria katika makanidhiano ya Vifaa hivyo

Afisa Mtendaji kata ya Mang’oto Bw.Mengi Chalamila akisoma taarifa ya Hali ya ukusanyaji wa Michango ilipofikia na hali ya ujenzi wa Bweni hilo unavyoendelea

Ndg.Burton Sinene kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Wilaya Idara ya Mipango akiwa kama Mjumbe wa Kamati ya Maafa akifafanua jambo

Award Mpandila Katibu wa MDA akiwapa pole wanafunzi waliounguliwa vifaa vyao vya shule ikiwa ni pamoja na nguo zao katika Ajali ya moto iliyotokea mwezi March mwaka huu

Makamu mwenyekiti wa MDA Ndg.Philipo Mahenge akimkabidhi Majina ya waliochangia vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh.Veronica Kessy

Award Mpandila Katibu wa MDA akimkabidhi Majina ya waliochangia vifaa hivyo Mkuu wa Shule ya Sekondari Mang’oto Mwl.Bonavetura Mgaya

Nembo ya Chama cha Maendeleo Makete yenye Kauli mbiu ya “Pamoja,tuijenge Makete yetu
Makamu mwenyekiti wa MDA Ndg.Philipo Mahenge akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh.Veronica Kessy vifaa vilivyonunuliwa na WanaMDA


Diwani Kata ya Mang’oto Mh. Osmundi Idawa akitoa neno lake la Shukrani kwa niaba ya ya wananchi kwa wote walioshiriki michango yao kupitia MDA

Wananchi wa Kijiji cha Makangalawe wakiimba wimbo wa Shukrani uliokuwa na ujumbe wa kushukuru kwa kile kilichotolewa na wanaMakete kupitia MDA



No comments

Powered by Blogger.