Header Ads

Waziri avutiwa na DC, Ammwagia sifa Kibao

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina amesifu utendaji kazi wa Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Godwin Gondwe katika usimamizi wenye weledi wa sheria za mifugo nchini

Luhaga ametoa sifa hizo kwa Gondwe akiwa kwenye ziara yake wilayani Handeni ambapo amekemea tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali katika Hifadhi za Misitu, Mapori ya Akiba na Serikali za Mitaa kukamata mifugo kiholela na kutoza faini zisizo na misingi ya kisheria.
“Ninamsifu mkuu wa Wilaya ya Handeni Ndugu Godwin Gondwe kwa utendaji wake mzuri na ripoti ya mifugo wilayani kwake ni nzuri lakini watendaji wa Serikali waliofanya hujuma na dhuluma kwa wafugaji hawatabaki salama, tutawafuatilia na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria” amesema Luhaga.
Waziri Mpina ameongeza kuwa jumla ya kaya milioni 4.49 za  kilimo nchini zinajishughulisha na ufugaji mifugo ya aina mbalimbali. Pia ameweka wazi kuwa kama sekta hiyo isingekuwa inazalisha mazao ya mifugo na Serikali kuamua kuagiza kutoka nje ya nchi basi ingelazimu kutumia kiasi cha sh. Trilioni 17.8.
Kwa upande wake Godwin Gondwe amesema pamoja na pongezi za Waziri Mpina, wao kama serikali ya Wilaya wataendelea kubuni mbinu mbalimbali za kuboresha sekta ya ufugaji ikiwemo uimarishaji wa majosho, malisho na uzuiaji uuzaji nyama kiholela barabarani.

No comments

Powered by Blogger.