Header Ads

KWA NINI MAKETE HATUFANIKIWI? Mwenyekiti MDA Clement Sanga

“Kusema kweli hii ni azma ambayo tunataka Makete tubadilike kwa nini sehemu zingine wameweza kufanikiwa? Why not us? Why not here? MDA tutalipigania hili kwa nguvu zote kwanza tunaanza na nyumbani” Clement Sanga
No automatic alt text available.
Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo Makete (MDA) Clement Sanga amesema Chama hicho kinatarajiwa kuwa Mkombozi kwa WanaMakete katika kubadili Maisha ya WanaMakete kwa kuwa hamasasisha wenye uwezo kifedha na kifikra kuwekeza Wilayani Makete

Akizungumza na Kitulo fm Mwenyekiti huyo amesema azma ya Chama hicho ni kubadili uhalisia wa Makete katika kuiendeleza kiuchumi,kijamii na kielimu kwa kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya Maendeleo ikizingatia Serikali ya awamu ya tano inatekeleza ahadi yake ya kuboresha miundombinu ya Barabara kwa kiwango cha Lami kutoka Njombe mpaka Makete
Ameongeza kuwa ili kuyafikia Maendeleo yanayotarajiwa ni lazima kila MwanaMakete mwenye moyo wa kupenda nyumbani aje awekeze nyumbani kwanza kuliko kuendelea kuwekeza maeneo mengine ilhali Makete kuna fursa nyingi za Uwekezaji

“Wafanyabiashara wengi wakubwa waliowekeza Mbeya,Dar es salaam,Tunduma na maeneo mengine wanaheshimika sana huko waliko,sasa hawa nao tunawaomba sana warudi pia kuwekeza kwao hapa nyumbani”


“Kusema kweli hii ni azma ambayo tunataka Makete tubadilike kwa nini sehemu zingine wameweza kufanikiwa? Why not us? Why not here? MDA tutalipigania hili kwa nguvu zote kwanza tunaanza na nyumbani” Ameongeza Sanga

Kwa upekee wake Chama hicho kimeweka Makao Makuu ya Chama Wilayani hapa huku kikitarajia kuanza kujenga Jengo la Chama Wilayani hapa kuanzia mwakani 2019

Wakati huohuo hivi sasa Chama hicho kimeunda Kamati mbili maalumu(Kamati ya Jamii na Kamati ya Uchumi na fedha) Kamati hizi zitahakikisha zinajihusisha na kufanya kazi kwa Karibu na Kila MwanaMakete aliyepo ndani na nje ya Makete katika kuhamisisha uwekezaji ndani ya Wilaya yake

Chama cha Maendeleo Makete mpaka sasa kinazaidi ya miaka miwili na wanachama wasiopungua 150

Chama hicho kinaendelea kupokea wanachama wapya na kujiunga kwa kiasi kidogo cha Fedha kwa mujibu wa Katiba ya Chama ni shilingi elfu 10 tu kwa mwaka,hivyo kwa yeyote anayehitaji kujiunga anaweza kuwasiliana na Viongozi wa Chama hicho ili kuijenga Makete pamoja

Katibu wa MDA- - -0768484715 (Award Mpandilah)
Naibu Katibu MDA- - -0715036902 (Monny Luvanda)

No comments

Powered by Blogger.