Header Ads

MBUNGE JIMBO LA MAKETE PROF.NORMAN SIGALLA KING AMEKABIDHI SHILINGI LAKI TANO NA BATI 50 UKARABATI WA MADARASA S/M TANDALA



Mbunge wa Jimbo la Makete Prof.NORMANI SIGALLA KING ametoa bati Hamsini pamoja na kiasi cha fedha Taslimu shilingi laki Tano na nusu  ilikusaidia ukarabati wa jengo moja katika shule ya Mazoezi Tandala iliyopo Kata ya Tandala Wilayani Makete Mkoani Njombe

Akikabidhi bati hizo hii leo kwa niaba ya Mbunge Katibu wa Mbunge FELIX KYANDO amesema Mbunge wa Jimbo la Makete ameamua kuongeza nguvu za wananchi wa Tandala kwenye ukarabati wa chumba kimojawapo cha Darasa shule ya Msingi Tandala kwa ajili ya kuhakikisha wanafunzi wanapata Elimu katika Mazingira rafiki kwa watoto

Pia Ndg.Felix Kyando ameongeza kuwa Mh.Mbunge ni mpenda maendeleo na yuko tayari kuunga mkono nguvu za wananchi katika shughuli za maendeleo hivyo Wananchi wa Makete watambue kwamba mwenye nacho huongezewa  ni vema na wao pia wakatoa nguvu zao kwenye suala zima la Maendeleo

Pia Mh.Mbunge mapema mwaka huu alikabidhi kiasi cha shilingi laki tano na nusu shuleni hapo kwa ajili ya ukarabati wa majengo shuleni hapo

Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Tandala Simoni Haule amemshukuru Mh.Mbunge wa Jimbo la Makete Prof.Normani Sigalla King kwa kujitolea kwake katika kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na wananchi wa Kata ya Tandala katika ukarabati wa jengo hilo

Mwl.Simoni Haule ameongeza kuwa wanatarajia kuezua paa la jengo lenye vyumba vitano vya Madarasa shuleni hapo ambalo linavuja hususani kipindi cha Masika na kulazimika kufanyia ukarabati wa kiwango cha juu sambamba na Ofisi moja ya walimu



No comments

Powered by Blogger.