Header Ads

WALEVI SAA ZA KAZI WILAYANI MAKETE KUKIONA


Image result for jeshi la polisi maketeJeshi la Polisi Wilayani Makete limewataka wananchi kuacha kunywa pombe kwa kupitiliza na kufuata muda wa kunywa pombe kisheria ambao ni kuanzia saa 10 jioni

Akizungumza na Kitulo fm Afande peter Suwi ambaye ni Operation officer Jeshi la polisi Wilaya ya Makete Mkoani Njombe amesema suala la watu kuvunja Sheria na kunywa pombe muda usiokubalika wataendelea kushughulikiwa kisheria kwa mujibu wa Sheria za nchi huku likitaja kijiji mojawapo cha Ivalalila kilichopo kata ya Iwawa ambacho wananchi wake wamekuwa wakivunja sheria ya unywaji wa Pombe

Jeshi hilo limesema kitendo cha watu kunywa pombe kuanzia asubuhi ni uvunjaji wa Sheria na kitendo hicho kunasababisha wananchi kushindwa kufanya shughuli za Maendeleo

"Sisi kama Jeshi la polisi tunataka watu wabadilike waache kunywa pombe saa za kazi na kuzingatia muda wa kuanza kunywa pombe haijalishi ni Klabu cha kuuza pombe za kinyeji au pombe kali"Aliongeza Afande Peter 

Pia Jeshi hilo Wilayani hapa limesema limejipanga vyema kuhakikisha Raia wake wanakuwa salama wakati wote wakifanya kazi za Maendeleo na hivi sasa Kituo cha Tandala kimeongezewa Askari Polisi pamoja na Gari jipya la Polisi limetolewa kwa ajili ya kuimarisha Ulinzi zaidi

Huku likijipanga kuweka kituo cha Polisi Kidogo kata ya Kitulo kijiji cha Ujuni kulingana na Matukio mbalimbali yanayotokea eneo hilo

"Tandala tumeongeza Askari Polisi wa kutosha lakini tumepeleka gari jipya kabisa pale kwa hivyo unaona ni namna gani vile tunataka Makete izidi kuwa salama,lakini pale ujuni kuna umuhimu mkubwa wa kuwepo kituo kidogo cha Polisi kulingana na mwingiliano mkubwa wa watu mbalimbali wanaoingia na kutoka kwa hiyo tupo kwenye mpango wa Haraka kufanya hivyo"Aliongeza

Kuhusu Kesi za Matukio ya Ubakaji na watu wazima kushiriki kimapenzi na wanafunzi na kusababisha Mimba Jeshi hilo limesema baadhi ya wazazi wanasababisha kesi hizo kutokuwa na nguvu na kuachiliwa kwa watuhumiwa jambo ambalo limekuwa changamoto kubwa katika utekelezaji wa sheria na kupambana na Mimba za utotoni

"Leo tu nilikuwa na Walimu wakuu wa Sekondari ya Lupila na Mang'oto kuhusu kesi hizohizo za wanafunzi (lakini hakutaja ni kesi gani)walimu wanalalamika kuhusu wazazi kumalizana na watuhumiwa majumbani kwao kwa hiyo inatuletea shida sana hii kuchukua sheria kwa watuhumiwa"

Sisi Polisi tunafurahi sana kuona mtu anahukumiwa kifungo hasa cha kwenda kutumikia jela lakini wazazi wanatuangusha pamoja na watoto wao,unakuta mtoto kituoni anatoa ushahidi vizuri tu lakini akifika Mahakamani anabadilisha alichokisema"



No comments

Powered by Blogger.