Header Ads

AFARIKI DUNIA KWA KUKANYAGWA NA GARI KIJIJI CHA IWAWA WILAYANI MAKETE


Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Aleso Mahenge(41) mkazi wa Iwawa amefariki Dunia kwa ajali ya kukanyagwa na Gari aina ya Isuzu Truck T597 AUW mwishoni mwa wiki iliyopita
Image result for JESHI LA POLISI
Ajali hiyo ilitokea mnamo tarehe 15 May 2018 saa 6 mchana kijiji cha Iwawa mtaa wa Dombwela akiwa kazini wakati wa kutengeneza kwenye Gereji ya Kumbuka Mahenge Wilayani Makete Mkoani Njombe

Mashuhuda wa Ajali hiyo wamesema Marehemu Aleso Mahenge alikuwa na wenzake wakisukuma gari hiyo lakini kwa bahati mbaya ikiwa na Dereva ndani yake iliserereka kwa nyuma na kumgonga Aleso ambaye alikanyagwa kwenye Mguu na kusbabisha Kupoteza uhai wake

Chrisantus Kavishe Kaimu Mkuu wa Polisi Wilaya ya Makete ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi Wilaya ameeleza kuwa Chanzo ya ajali hiyo ni Dereva kukosa Umakini wa kulimudu gari

Dereva huyo aliyetambulika kwa jina la Orgeni Mtenzi (42) mkazi wa Iwawa Wilayani hapa amekamatwa na atafikishwa Mahakamani pindi ushahidi utakapokamilika na Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo

No comments

Powered by Blogger.