MBUNGE ATAKA AJIRA KWA VIJANA WA MAKETE UJENZI WA LAMI
Mbunge wa Jimbo la Makete Prof.Norman Sigalla King ameitaka Kampuni ya Kichina inayotekeleza Ujenzi wa Mradi wa Barabara kwa kiwango cha Lami kipande cha kutoka Moronga,Ndulamo-Makete kuhakikisha inatoa ajira kwa vijana wa Makete kulingana na Mahitaji yao
Akizungumza na Viongozi wanaosimamia utekelezaji wa Mradi huo Prof.Norman Sigalla King alipotembelea Kambi ya Kampuni hiyo na kutembelea baadhi ya Maeneo kuangalia shughuli ya ujenzi inavyoendelea amesema ni vema ajira zinazohitaji taaluma kama Vijana wa Makete wapo wenye taaluma hiyo basi waajiriwe zile ajira ya vibarua ziwanufaishe vijana wa Makete
Kampuni hiyo inayotekeleza Mradi huo imesema kwa kipindi cha Masika ajira zilikuwa chache kwa Vijana lakini kwa kipindi hiki ambacho mvua zimepungua na kuelekea kiangazi ajira zaidi zitatolewa kwa Vijana hususani WanaMakete kwa kuzingatia weledi wao kitaaluma na ajira za vibarua bila ubaguzi
Kampuni hiyo imesema kwa sasa tayari imeanza kupokea barua nyingi za Maombi ya kazi zilizoandikwa na vijana wakiomba Ajira na kuongeza kwamba waliotuma maombi tayari watapewa kipaumbele zaidi
Wakati huohuo Prof.Norman Sigalla King ameipongeza Kampuni hiyo kwa kasi yao kwenye utekelezaji wa Mradi huo unaotegemea kukamilika kwa kipindi cha miaka miwili na nusu
Lakini Kampuni inayotekeleza Mradi huo imesema inatarajia mradi huo ukamilike kabla ya muda uliopangwa wa miaka miwili na nusu katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya usafiri kufuatia uwepo wa Miundombinu imara ya barabara
Katika picha Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Makete Prof.Norman Sigalla King akiwa na mmoja wa wasimamizi Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Lami kipande cha kutoka Moronga kuelekea Ndulamo-Makete Mjini
Vijana wazawa wa Makete waliojipatia Ajira kwenye Kampuni ya Ujenzi ya China inayojenga Barabara ya Lami Kipande cha Moronga,Ndulamo-Makete wakiwa kwenye ujenzi wa Daraja lililopo kijiji cha Ikonda Kata ya Tandala
No comments