Header Ads

WANAUME WATAKIWA KUWA WAVUMILIVU KWA WAKE ZAO


Wanawake kwa Wanaume Wilayani Makete Mkoani Njombe wametakiwa kuwahi Hospitali mara wanapoona dalili za hatari kwa mama Mjamzito ili kupatiwa matibabu.

ROSEMERY LUVANDA ni muuguzi Hospitali ya Wilaya ya Makete Kitengo cha Mama na Mtoto amesema kuwa Wanaume na wanawake wanapoona dalili za hatari kwa mama mjamzito wanatakiwa kuwahi kufika katika kituo chochote cha kutolea huduma za Afya ili kupata elimu juu ya dalili za awali zinavyotokea kwa mama Mjamzito.

BI.ROSEMERY ameiomba Jamii ya Wanamakete kutambua dalili za hatari anazoweza kuzipata mama Mjamzito ikiwa ni pamoja na maumivu ya kichwa, kuumwa kwa tumbo chini ya kitovu,pamoja na kujisikia kizunguzungu ambacho husababishwa upungufu wa damu.

ALAMOKA MAHENGE ni mama Mjamzito kutoka Kijiji cha Iwawa Mamlaka ya Mjimdogo wa Iwawa amewataka wanaume kuwajibika kuwasindikiza wake zao Klinic   mara wanapoona mwanamke ni mjamzito ili kupata elimu juu ya dalili za hatari kwa mama mjamzito na amewataka wanaume kuwa na uvumilivu pindi mama anapokuwa mjamzito .


No comments

Powered by Blogger.