Header Ads

MWANAFUNZI ASHIKILIWA NA POLISI MAKETE KWA KUTUHUMIWA KUCHOMA BWENI LA WAVULANA MANG'OTO SEKONDARI

 Mwonekano wa Bweni hilo baada ya kuungua


 Wananchi waliofika kushuhudia Ajali hiyo ya moto



 Baadhi ya vitu vilivyookolewa
 Haya ndiyo Magodoro yaliyookolewa ambayo ni manne tu

Wanafunzi shule ya Sekondari Mang'oto wakimsikiliza Afisa Elimu Sekondari Mwl.Jacob Meena aliyefika shuleni hapo na kuzungumza na Wanafunzi hao


Mwanafunzi wa kidato cha pili Mvulana (15) jina linahifadhiwa amekiri kuchoma Bweni la Wavulana shule ya Sekondari Mang'oto kwa madai kuwa amechukizwa na adhabu aliyopewa na Wanafunzi wenzake ya kupigwa baada ya kubomoa kibanda cha Mwalimu na kuiba pipi,Biskuti na karanga hapo Juzi Jumapili 

Baada ya kupewa adhabu hiyo mwanafunzi huyo amesema aliamua kurudi kijijini kwao Makangalawe na jana aliporudi shule alirudi akiwa na Mpango wa kuchoma Bweni akiwa na kiberiti

Mwanafunzi huyo amesema amechoma bweni hilo mnamo saa moja jioni wakati wanafunzi wenzake wakiwa Darasani vipindi vya usiku

Wanafunzi wakiwa Darasani wakaona kama Bwenini kuna moto ndipo walipogundua tukio hilo na kupiga yowe kuomba msaada


Mwanafunzi wa kwanza kujua tukio hilo na aliyemkata Mwanafunzi huyo ameelezea alichokishuhudia na kuongeza kuwa wakati huo ndani ya Bweni kulikuwa na wanafunzi kadhaa walikuwa wamejipumzisha ambao ni wagonjwa lakini walikuwa hawajui kama nje Bweni linaungua

Afisa Elimu Sekondari Mwl.Jackob Meena amewaomba wanafunzi kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu kwao wakati utaratibu ukiendelea kufanyika ili kuwasaidia wanafunzi waliounguliwa na vifaa vyao


Wananchi waliofika kushuhudia Ajali hiyo wamesema Ajali hiyo imewasikitisha lakini wanashukuru kwamba wanafunzi wote wako salama

Diwani wa Kata ya Mang’oto Mh.Osmund Idawa ametoa pole kwa wanafunzi hao na wazazi kufuatia kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa baada ya tathmini kufanyika yupo tayari kushirikiana na wazazi kurudisha miundombinu ya Bweni hilo

Bweni hilo linabeba wanafunzi zaidi ya 140 na ni magodoro manne tu yaliyookolewa huku vitu vingine vikiwa vimeteketea kabisa

No comments

Powered by Blogger.