MIMBA ZA UTOTONI NA MATUKIO YA UBAKAJI BADO NI TATIZO MAKETE
Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh.Veronica Kessy ameelezea kukerwa na mimba za watoto wa kike zinazopelekea kutokuendelea na masomo yao.
Mh.Veronica Kessy ameelezea hayo akiwa Kata ya Lupila kijiji cha Lupila Wilayani Makete Mkoani Njombe akiongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh.SUZAN KOLIMBA mapema wiki hii .
Mh.Kessy amesema baadhi ya wazazi wamekuwa na tabia za kumalizana na kuwafundisha watoto hao kutoa ushahidi wa uongo mara kesi hizo zinapofikishwa kwenye vyombo vya sheria ikiwemo Mahakama.
''Ninyi wazazi mnawajenga Vibaya sana hawa watoto wa kike,akipata Mimba mnamalizana Kifamilia,mnakubaliana na kufunika jambo hili na akipelekwa Mahakamani mnamwambia akamtaje mtu mwingine tena isitoshe mtu asiyejulikana''Amesema Veronica Kessy.
"Wanamakete tafadhali nawaomba sana Mimi naumia kama Mama kwanza tunawapeleka Mabinti wadogo kwenda kuishi maisha ya kikubwa ambao hawajafikia umri,Hata kama ni mila na Desturi jamani Tufunguke tuione Dunia inakwenda wapi".
Pia amewaomba wazazi hao kutekeleza majukumu yao ya msingi ya kuwapatia watoto wa kike elimu kwani 50 kwa 50 itafika mahala itakusekana bila elimu amesema kwa bahati nzur sasa elimu ni bure.
Kwa Mujibu wa KituloRedio Fm kupitia Kampeni yake ya "Niache Nisome Mzazi Timiza wajibu wako"Takwimu zinazonesha kwamba kwa mwaka jana 2017 wanafunzi 20 wameachishwa Masomo kwa kupata ujauzito wakiwa shuleni na wanafunzi wawili(2) wakiwa shule ya Msingi jambo linalohatarisha na kufifisha ndoto za Wanafunzi hao.
Wakati huohuo Matukio 15 ya ubakaji yameripotiwa katika kipindi cha mwaka jana Wilayani Makete Mkoani Njombe
No comments